Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Aprili 26, 2024 Local time: 06:29

Ghasia zakumba Tunisia


Waandamanaji nchini Tunisia baada ya kuuawa kwa kiongozi wa upinzani Chokri Belaid, Februari 7,2013
Waandamanaji nchini Tunisia baada ya kuuawa kwa kiongozi wa upinzani Chokri Belaid, Februari 7,2013

Mkosoaji huyo mkubwa wa serikali alipigwa risasi kadhaa akitoka nyumbani kwake Jumatano.


Chama kikuu cha wafanyakazi huko Tunisia kimeitisha mgomo wa kitaifa Ijumaa, ili waungane na waombolezaji kwenye mazishi ya kiongozi wa upinzani aliyeuawa Chokri Belaid .

Mgomo huo ulitangazwa Alhamisi usiku na umoja wa vyama vya wafanyakazi wa Tunis, na kuzusha ghasia za kisiasa ambazo zilipelekea chama tawala cha kiislam kukataa mpango uliowekwa na waziri mkuu wake kuunda serikali mpya.Polisi wa kutuliza ghasia pia walipambana na waandamanaji kwenye mji mkuu kwa siku ya pili.

Waziri mkuu Hamadi Jebali alitangaza Jumatano usiku mpango wake wa kufuta serikali ya sasa baada ya ghasia kulipuka katika mji mkuu kufuatia kuuwawa kwa Belaid.
Alisema serikali mpya itajumwisha wataalam wasiokuwa na uhusiano wowote na vyama vya kisiasa. Tangazo hilo lilipokelewa kwa furaha kubwa na viongozi wa upinzani.

Watu wasiojulikana walimpiga risasi mara kadhaa mkosoaji huyo mkubwa wa serikali, alipokuwa akiondoka nyumbani kwake Jumatano. Kufikia sasa hakuna mtu aliyekamatwa kuhusiana na kifo chake.
XS
SM
MD
LG