Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Mei 02, 2024 Local time: 01:02

Israel na Hamas zasitisha mapigano.


Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Hillary Clinton akiwa na waziri wa mambo ya nje wa Misri Mohammed Kamel Amr, wakitangaza sitisho la mapigano kati ya Israel na Hamas huko Cairo Misri,Jumatano, Nov21,2012.
Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Hillary Clinton akiwa na waziri wa mambo ya nje wa Misri Mohammed Kamel Amr, wakitangaza sitisho la mapigano kati ya Israel na Hamas huko Cairo Misri,Jumatano, Nov21,2012.
Misri imetangaza makubaliano ya kusitisha mapigano kati ya ya Israel na Hamas, itakayoanza saa tatu usiku za Mashariki ya Kati.

Waziri wa mambo ya nje wa Misri Mohamed Kamal alitoa tangazo la kusitisha mapigano huko Cairo Jumatano usiku akiwa pamoja na waziri wa mambo ya nje wa Marekani Hillary Clinton pembeni yake .

Masharti ya kusitisha mapigano ni pamoja na pande zote mbili kusitisha uhasama na kufunguliwa maeneo ya mpaka kutoka Gaza ili kuruhusu usafirishaji wa bidhaa na watu . Kutakuwa na kipindi cha saa 24 cha kutekeleza usitishaji mapigano. Misri itasimamia na kufuatilia ukiukaji wowote utakaofanya na pande zote mbili.

Makubaliano hayo yamefikiwa baada ya saa kadhaa za mazungumzo ya kidiplomasia ya kusafiri sehemu moja hadi nyingine yaliyomhusisha waziri Clinton pamoja na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki Moon.

Clinton amesema makubaliano hayo ni ‘tukio muhimu sana kwa eneo hilo.”
XS
SM
MD
LG