Polisi nchini Ufaransa Ijumaa walimpiga risasi mtu aliyekuwa na silaha ambaye alikuwa anajaribu kuwasha moto katika sinagogi katika mji wa kaskazini wa Rouen.
Moshi ulikuwa umesambaa katika eneo la mpakani la kaskazini mwa Israel Alhamisi (Mei 16) baada ya msururu wa makombora kufyatuliwa kutoka Lebanon na kupiga maeneo ambayo hayana watu, huku Hezbollah ikiwa inafanya mashambulizi kwa kutumia droni na makombora yanayopigwa bila ya shabaha.
Kikundi cha Wafilipino kinachoongoza juhudi ya kusambaza mahitaji muhimu katika Bahari ya South China kimefikisha chakula na mafuta kwa wavuvi wa Ufilipino licha ya kufuatiliwa na vyombo vya majini vya China, maafisa wake walisema Alhamisi, wakiita ni “ushindi mkubwa.”
EU na Marekani walielezea wasiwasi wao wiki hii kufuatia kukamatwa kwa waandishi, wachambuzi wa kisiasa na wanasheria.
Baraza la Katiba lililotangaza ushindi huo pia lilikataa ombi lililotolewa na Waziri Mkuu Succes Masra la kutaka kufutwa matokeo hayo.
Rais Zelenskyy alisafiri Alhamisi kwenda Kharkiv kukutana na maafisa wa kijeshi huku mashambulizi ya Russia yakifanyika katika mkoa huo.
Hii itaashiria mabadiliko ya haraka kuliko kesi nyingi zilizo katika mfumo wa uhamiaji Marekani zinazochukua muda mrefu
Balozi wa Afrika Kusini nchini Uholanzi amelisihi jopo la majaji 15 wa kimataifa kuiamuru Israel iondoke bila masharti huko Gaza.
Vikosi vya Israel mapema mwezi huu vilichukua udhibiti wa upande wa Gaza wa mpaka wa Rafah na Misri.
Niger ambayo haina bahari mwaka jana ilizindua bomba la kusafirisha mafuta ghafi kutoka kwenye kinu chake kupitia CNPC.
Tangazo hilo linakuja wakati wanajeshi wa Ukraine wakirejea kaskazini mashariki mwa nchi hiyo kufuatia mapigano
Timu ya wataalamu 19 wa afya wakiwemo Wamarekani 10 imekataliwa kuondoka Gaza baada ya kutoa huduma za matibabu
Pandisha zaidi