Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Aprili 26, 2024 Local time: 13:30

Waislam washerekekea Eid al-Fitr


Waislam wakiswali msikitini Bamako, Mali Agosti 8, 2013.
Waislam wakiswali msikitini Bamako, Mali Agosti 8, 2013.
Waislam duniani kote wanasheherekea sikukuu ya Eid al Fitr Alhamis wakiadhimisha kumalizika kwa mwezi mtukufu wa Ramadhan.

Waumini walikusanyika katika misikiti huko Indonesia nchi yenye waislam wengi kuliko zote duniani kwa sikukuu hiyo ya Eid leo.

Sherehe za Eid pia ziliadhimishwa Saudi Arabia, Syria na Malaysia.
Nchini Misri, makundi ya waumini waliomba na kusheherekea katika uwanja wa Tahrir Square, wakati viongozi wa muda wa Misri wakihudhuria sala ya Eid katika mji huo mkuu.

Waislam huko Kenya na Tanzania wanasherehekea siku kuu hiyo ya Eid al-Fitr kesho Ijumaa
XS
SM
MD
LG