Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Mei 18, 2024 Local time: 21:37

UN, EU na marekani zimetoa wito wa kusitishwa mapigano nchini Sudan


jenerali wa Kikosi cha RSF, Mohamed Hamdan Daglo (kulia) na Jenerali wa jeshi la Sudan Abdel Fattah al –Burhan ( kushoto). Picha na AFP.
jenerali wa Kikosi cha RSF, Mohamed Hamdan Daglo (kulia) na Jenerali wa jeshi la Sudan Abdel Fattah al –Burhan ( kushoto). Picha na AFP.

Mvutano wa muda mrefu ulizuka na kuanzisha mapigano ya mitaani katika mji mkuu Khartoumna maeneo mengine ikiwemo jimbo la magharibi mwa Darfur.

Umoja wa Afrika, Umoja wa Ulaya na Marekani zimetoa wito Alhamis wa kusitishwa mara moja kwa mapigano na kupanga mazungumzo kati ya makundi yanayohasimiana nchini Sudan.

Makundi hayo pia yalitoa wito wa kusitishwa kwa mvutano kati ya Somalia na Ethiopia kufuatana na makubaliano yaliyotiwa saini kati ya Ethiopia na Somaliland, jimbo lililojitenga na Somalia.

Wawakilishi wa makundi hayo, ambao walizungumza mjini Kampala, Uganda, baada ya mkutano wa jumuiya ya kikanda ya Afrika Mashariki na Pembe mwa Afrika IGAD, wamesema kuwa migogoro hiyo miwili inatishia utulivu wa kikanda katika Pembe ya Afrika.

Vikosi vya jeshi la Sudan na hasimu wake Kikosi cha Dharura RSF vimekuwa vikipigania udhibiti wa Sudan tangu mwezi Aprili. Mvutano wa muda mrefu ulizuka na kuanzisha mapigano ya mitaani katika mji mkuu Khartoumna maeneo mengine ikiwemo jimbo la magharibi mwa Darfur.

Forum

XS
SM
MD
LG