Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Aprili 26, 2024 Local time: 23:04

Umoja wa Mataifa unaadhimisha siku ya Walinda Amani


Walinda amani wa Umiojja wa mataifa wakifanya doria huko el Fasher Sudan.
Walinda amani wa Umiojja wa mataifa wakifanya doria huko el Fasher Sudan.
Wakati dunia inaadhimisha siku ya walinda amani duniani mei Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon amesema Umoja huo kamwe hautasahau gharama za kijamii ambazo familia inakumbana nazo pindi jamaa au ndugu zao wanapojitolea mhanga kulinda amani duniani. Taarifa zaidi na Assumpta Massoi.

Kumbukumbu maalum ya walinzi wa amani wa Umoja wa Mataifa waliopoteza maisha yao sehemu mbali mbali duniani wakitetea misingi ya Umoja huo iliongozwa mjini New York, na katibu Mkuu Ban Ki-Moon.

Baada ya dakika moja ya ukimya, alizungumza na kueleza kuwa tangu kuanza Umoja wa Mataifa uanze kupeleka walinzi wa amani miaka 65 iliyopita, walinda amani Elfu Tatu wamekufa kwa sababu mbali mbali na mwaka jana pekee waliokufa ni 111.

Bwana Ban pamoja na kutuma rambirambi kwa familia na jamaa, amesema wanachofanya sasa ni kuimarisha ulinzi wa watendaji hao duniani kote.

Kikosi kikubwa kabisa cha kuklinda amani kwa wakati huu ni kile cha MONUSCO, kilichoko huko Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo kimeadhimisha siku kwa kuwakumbuka walinda amani 150 walipoteza maisha yao katika juhudi za amani mnamo kipindi cha miaka 10 iliopita nchini DRC.

wakati wa sherehe hizo MONUSCO imesema wapiganaji 91 wakiwemo wale wa kundi la M23 walijisalimisha mnamo kipindi cha wiki mbili jimboni Kivu ya kasakazini.

MONUSCO ya adhimisha siku ya walinda amani - 1:59
please wait

No media source currently available

0:00 0:01:59 0:00
Kiungo cha moja kwa moja

Luteni kanali, Felix Basse,msemaji wa MONUSO, amewambia wandishi habari mjini Kinshasa siku ya Jumatano kwamba Kongo ni miongoni mwa nchi ambazo zinaidadi kubwa ya wanajeshi wa umoja wa mataifa waliopoteza maisha yao katika juhudi za kulinda amani:

“Toka enzi ya MONUC na kufikia MONUSCO hivi sasa,wanajeshi wetu 149 wamekufa hapa nchini Kongo, hata hivyo juhudi za kutafuta amani zitaendelea .Siku ya leo ni ya kuwapa pia moyo wanajeshi zaidi ya laki moja wanaofanya kazi chini ya bendera ya Umoja wa Mataifa”.

Hata hivyo Felix Basse amesema kwamba idadi hiyo ya wanajeshi waliofariki hapa nchini haimaniishi kwamba waliuliwa wote na wapiganaji, bali idadi kubwa inatokana na ajali za ndege, na za barabani.

Sherehe kadhaa zimefanyiaka hapa mjini Kinshasa ilikuadjimisha siku kuu hiyo ya wanajeshi wa umoja wa mataifa. Mada kuu ya siku kuu hiyo ni kujiambatanisha na change moto mpya za ulinzi wa amani.

Kwenye mkutano na wandhi habari hapa mjini Kinshasa hapa mjini inshasa msemaji wakijeshi wa tume ya MONUSCO,alisema kwamba ijapokuwa change moto nyingi wanazokabilana nazo lakini wanajeshi wa MONUSO wataendelea na shuruli zao za kuwakinga raia wa Kongo.

Amesema mnamo kipindi cha wiki mbili wapiganaji 91 kutoka makundi tofauti ya wapiganaji wamejisalimisha jimboni Kivu

“Wapiganaji hao walijisalimisha kwenye vituo vyetu vya operesheni vilivyoko kwenye uwanja wa ndege wa Goma,mjini sakae, Rutshuru, Nyanzale, Mugunga Rwindi, Mpati, Katale, Nyamilima na Kiwanja. Miongoni mwa wapiganaji hao kuna wale wa M23 19 na 45 kutoka makundi ya wapiganaji Maimai”.

Luteni Kanali Felix Basse amesema kwamba roketi zilizoanguka mjini Goma na Mugumba ambazo ziliwauwa watu wasiopunguwa wawili na kuwajeruhi wengine kadhaa zilirushwa na wapiganaji wa M23 walioko Kibati.
XS
SM
MD
LG