Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Mei 17, 2024 Local time: 14:36

Ukraine yasema mustakabali wa vita unategemea mashambulizi ya ndege zisizo na rubani


Waziri wa mabadiliko ya Digitali wa Ukraine Fedorov akizungumza wakati wa mahojiano na Reuters.
Waziri wa mabadiliko ya Digitali wa Ukraine Fedorov akizungumza wakati wa mahojiano na Reuters.

Waziri anaesimamia Mabadiliko ya Kidijitali nchini Ukraine Mykhailo Fedorov amesema kwamba mustakabali wa vita vya Ukraine dhidi ya Russia unategemea mashambulizi mengi yatakayofanywa na ndege zisizo na rubani.

Akizungumza na shirika la habari la Reuters kwamba hali hiyo itategemea pia na kuwepo na mashambulizi machache ya meli za Russia.

Fedorov alisema utengenezaji wa ndege zisizo na rubani za Ukraine umeongezeka kwa zaidi ya mara 100 tangu mwaka jana.

Fedorov pia aliliambia Reuters kwamba Ukraine inafanyia majaribio mifumo ya teknolojia ya AI, ambayo inaweza kutambua shabaha kwa umbali umbali wa kilomita kadhaa, pamoja na vifaa vinavyoongoza ndege zisizo na rubani licha ya kuharibiwa nmitambo ya kivita ya kielektroniki.

Wakati huo huo, Wizara ya Ulinzi ya Uingereza, katika taarifa zake za kijasusi za kila siku kuhusu Ukraine, ilisema kuna uwezekano kwamba Russia itaanza tena kutumia makombora ya masafa marefu ili kulenga miundombinu ya Ukraine wakati wa baridi.

Forum

XS
SM
MD
LG