Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Aprili 26, 2024 Local time: 06:36

Jeshi la Umoja wa Mataifa litadumaza uhuru wa Sudan Kusini-Michael Makuei


Waziri wa habari wa Sudan Kusini Michael Makuei Lueth akizungumza kwenye mkutano mjini Addis Ababa, Jan. 5, 2014.
Waziri wa habari wa Sudan Kusini Michael Makuei Lueth akizungumza kwenye mkutano mjini Addis Ababa, Jan. 5, 2014.

Serikali ya Sudan Kusini inasema inapinga rasimu ya azimio lililodhaminiwa na Marekani ambalo limesambazwa kwenye baraza la usalama la Umoja wa mataifa kwa ajili ya kupeleka vikosi huko Juba na maeneo ya nchi yaliogubikwa na ghasia.

Waziri wa habari wa serikali ya Juba Michael Makuei amesema jeshi kama hilo halikubaliki kama litasimamiwa na tume ya Umoja wa mataifa nchini Sudan Kusini na litadumaza uhuru wa Sudan Kusini.

“Ni haki yetu kupinga na kama watu wakiamua kulazimisha basi itakuwa nje ya mkutano mkuu na nyaraka zozote za umoja wa mataifa na za kanda zote, hakuna mahali popote duniani ambapo unaweza kulazimisha ndio tunafahamu marekani wakati mwingine inafanya maamuzi ya peke yake kwasababu ni nchi yenye nguvu duniani” aliongeza.

Baraza la usalama la Umoja wa mataifa limeongeza muda kwa jeshi la la kulinda amani -UNMISS ambao muda wake unakaribia kwisha mpaka Ijumaa hii. Viongozi wa nchi katika kanda hiyo wamekuwa wakikutana mjini Addis Ababa kujadili mpendekezo ya jeshi hilo la kulinda amani.

XS
SM
MD
LG