Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Mei 08, 2024 Local time: 08:07

Galaxy Note 7 yapigwa marufuku ndani ya ndege


Samsung Gadgets Galaxy Note7
Samsung Gadgets Galaxy Note7

Wizara ya usafirishaji Marekani imepiga marufuku simu ya aina ya Samsung Galaxy Note 7 katika safari zote za ndege ndani ya Marekani baada ya matukio karibu 100 ya simu hiyo kupata joto la kupita kiasi na mara nyingine kulipuka.

Idara ya safari za anga -FAA- ya Marekani awali ilihimiza wasafiri kuzima simu hizo wakiwa ndani ya ndege, na kuziweka katika masanduku wakati wa safari. Lakini marufuku hii mpya inakataza hata simu zilizozimwa ndani ya ndege na itaanza kutekelezwa Jumamosi mchana kwa saa za Marekani.

Kampuni ya Korea Kusini inayotengeneza simu hiyo inasema inawasiliana na wenye simu hizo kuwaelekeza kuhusu marufuku hiyo. Kampuni hiyo ilitangaza Jumatatu kuwa inasimamisha kutengeneza simu ya Galaxy Note 7 baada ya simu hizo kushika joto na nyingine kulipuka.

XS
SM
MD
LG