Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Aprili 29, 2024 Local time: 12:09

Rwanda kuruhusu wageni kutoka mataifa ya Afrika kuingia bila Visa


Rais wa Rwanda Paul Kagame
Rais wa Rwanda Paul Kagame

Rwanda Alhamisi imetangaza kwamba itawaruhusu waafrika kuingia nchini humo bila ya visa, likiwa taifa la karibuni la katika bara hilo kuchukua hatua inayolenga kuimarisha usafiri wa watu na bidhaa, sawa na ilivyo barani Ulaya kwenye eneo la Schengen.

Kwa mujibu wa shirika la habari la AP, rais wa taifa hilo Paul Kagame alitoa tangazo hilo katika mji mkuu wa Kigali, ambapo alihimiza uwezo wa Afrika kama kivutio cha utalii wa ndani, kinyume na kutegemea asilimia 60 ya watalii kutoka nje, kulingana na data kutoka shirika la Umoja wa Mataifa la Kiuchumi na Afrika.

Muafrika yeyote anaweza kuchukua ndege na kuingia Rwanda pale anapotaka, bila kulipia chochote, amesema Kagame wakati wa kongamano la 23 la Kimataifa la Baraza la Usafiri na Utalii. Iwapo hilo litatekelezwa, Rwanda itakuwa taifa la nne la kiafrika kutangaza hatua hiyo baada ya Gambia, Benin, na Ushelisheli.

Rais wa Kenya William Ruto mapema wiki hii alitangaza mpango wa kuruhusu waafrika kutembelea taifa hilo la Afrika Mashariki bila kulipia visa, ifikapo Decemba 31.

Forum

XS
SM
MD
LG