Wapiga kura katika jimbo la Michigan nchini Marekani wanapiga kura leo Jumanne katika uchaguzi wa awali wa kumpata mgombea urais wa chama cha Democratic na Republican huku rais Joe Biden na rais wa zamani Donald Trump wakitarajiwa kushinda.
Kiwango cha ushindi huo kitaangaliwa kwa karibu kama ishara za kuungwa mkono kwa wagombea hao wawili katika jimbo hilo muhimu, ambao wanatazamiwa kurejesha mtazamo wa ushindani waliokuwa nao katika uchaguzi wa urais wa mwaka 2020 ambapo Biden alishinda.
Michigan ni makazi ya mkusanyiko mkubwa wa Wamarekani wenye asili ya Kiarabu, na kuna upinzani dhidi ya utawala wa Biden kuunga mkono vita vya Israel huko Gaza umesababisha baadhi ya Wa-Democrat kuwataka wapiga kura kutoegemea kokote kwa upigaji kura wa leo Jumanne badala ya kupiga kura kwa Biden.
Trump ameshinda kila jimbo hadi sasa katika kinyang'anyiro cha uteuzi wa chama cha Republican, na kura za maoni katika jimbo la Michigan zilimuonyesha akiwa anaongoza kwa alama za juu katika jimbo hilo.
Forum