Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Mei 22, 2024 Local time: 01:15

Marekani yajitayarisha kwa ongezeko la wahamiaji wakijaribu kuingia nchini


Wahamiaji waliowasili wakijaribu kuingia kupitia mpaka wa Mexico na Marekani
Wahamiaji waliowasili wakijaribu kuingia kupitia mpaka wa Mexico na Marekani

Marekani inajitayarisha kwa ongezeko la wahamiaji wanaojaribu kuvuka mpaka upande wa kusini mwa taifa la Marekani.

kufuatia kumalizika kwa Title 42 siku ya Alhamisi, sera ambayo inahusishwa na janga iliyoiruhusu Marekani kuwafukuza wahamiaji zaidi ya mara milioni 2.8, kwa mujibu wa makundi yaliyokuwa yanafutilia.

White House ambayo inalaumiwa kwa picha za vurugu kwenye mpaka, inajitetea dhidi ya ukosoaji na kusema Bunge linahitaji kuchukua hatua.

White House ilifanyakazi kushughulikia wasi wasi kwamba matukio kama hayo huenda yakawa ni kawaida kwenye mpaka wa kusini wakati Title 42 itakapoondolewa.

Afisa wa ngazi ya juu wa uhamiaji wa Rais Joe Biden Jumatano alitangaza kanuni mpya inayohusu wahamiaji ambao wanavuka mpaka kwenye maeneo ya kuingia, haraka wataondolewa na hawastahili kupewa hifadhi, isipokuwa kupitia app ya CBPone ambayo itaendelea kutoa ulinzi kwa waomba hifadhi.

Waziri wa Usalama wa Ndani wa Marekani, Alejandro Mayorkas, anasema, “kama mtu yeyote anawasili kwenye mpaka wetu wa Kusini baada ya saa sita usiku leo, ataonekana kuwa hawastahili kupewa hifadhi na atashuhhulikiwa kikamilifu kwa kuingia nchini kinyume cha sheria, ikiwemo marufuku ya takriban miaka mitano kuingia tena na uwezekano wa kushtakiwa kwa uhalifu.”

Biden anasema Bunge linahitaji kufanya mengi zaidi. “Nimeliomba Bunge kufanya mengi zaidi kwa ajili ya Ulinzi wa Mpakani. Hawakufanya hivyo. Wameifanya iwe vigumu.”

Wapinzani wa Biden wanasema hafanyi vya kutosha kuwaweka wamarekani salama.

Mbunge Joe Wilson, Mrepublican anasema “Sera za Biden za mpaka zinadumaza ulinzi wa taifa na kuzihatarisha familia za wamarekani kila mahali kwa shambulizi la kigaidi litakalofanywa na wageni.”

Lakini watetezi wa uhamiaji wanasema mfumo wa Biden ni mkali sana.

Melissa Crow wa Kituo cha Masuala ya Jinsia na Wakimbizi anasema “kanuni hii itahatarisha siyo tu maisha ya watu wanaotafuta usalama bali italeta vurugu zaidi na matatizo katika mpaka wetu wa kusini. Kama utawala unavyofahamu vyema, pia ni dhahiri ni kinyume cha sheria. Kimsingi, kanuni mpya inachanganya na kujumuisha marufuku mbili za enzi ya Trump ambazo Rais Biden mwenyewe alizikana katika kampeni yake, na zote mbili zilifutwa kuwa ni kinyume cha sheria katika mahakama ya serikali kuu.” Utawala haukubaliani.

Waziri wa Usalama wa Ndani anasema Rais ameongoza upanuzi usio na kifani wa njia halali na kwamba wako tofauti na utawala uliopita.

Wakati mjadala ukiendelea hapa Washington, hakuna dalili kuwa Bunge lililogawanyika katika nchi litakubaliana na sera mpya kuzungumzia idadi ya wahamiaji wenye ama ya kuwa na maisha mapya nchini Marekani.

XS
SM
MD
LG