Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Mei 02, 2024 Local time: 00:59

Mwanamuziki wa Afrika Kusini awatumbwiza watu katika sherehe za kuapishwa Obama


Lira akiimba katika tamasha la kusherehekea kuapishwa kwa rais Obama
Lira akiimba katika tamasha la kusherehekea kuapishwa kwa rais Obama
Maelfu ya watu walimiminika katika jiji la Washington kuhudhuria kuapishwa kwa rais Barack Obama kwa mhula wa pili lakini zaidi pia walikuja kusherehekea katiaka tamasha mbali mbali zilizofanyika kote katika mji mkuu wa Marekani.

Miongoni mwa wasani mashuhuri wa Afrika alikuwepo Lira kutoka Afrika Kusini. Aliimba katika sherehe za kwanza kuandaliwa ubalozi wa nchi mbali mbali za dunia ili kusherehekea pamoja na rais Obama na kusisitza umuhimu wa uhusiano wa kimataifa.

Ingawa rais hakuhudhuria tamasha hiyo Lira alimuimbia nyimbo maalum ambayo aliwahi kumuimbia rais wa zamani Nelson Mandela wakati wa kuadhimisha miaka 92 ya kuzaliwa kwake. “Something inside so strong.”
Lira mwimbaji chipikizi wa Afrika Kusini
please wait

No media source currently available

0:00 0:05:39 0:00


Lira anasema amefurahi kualikwa na kuhudhuria sherehe hizo ingawa hafahamu jinisi alivyoalikwa. “Mwanzoni mimi sikufahamu jinsi ilivyotokea. Tulipata barua pepe kueleza kwamba kuna tamasha inafanyika na wangelipenda tushiriki katika tamasha hilo. Basi mimi ninadhani ni jambo kubwa kuweza kuhudhuria na kuwepo hapa DC wakati wa sherehe za kuapishwa Obama.”

Baada ya kumsikiliza na sauti yake nyororo yakuvutia nimefahamu kwanini alialikwa. Akiwa na umri wa miaka 33 Lira ambae jina lake la kuzaliwa ni Lerato Molapo, ameshatoa albamu sita, nne akirikodi katika studio na mbili akiwa katika tamasha. Pamoja na dvd mbili, na ameshajinyakulia tunzo kadhaa nyumbani na kimataifa.

Lira anasema muziki wake ambao yeye huandika na kutunga mweneywe kwa lugha nne tofauti za Afrika Kusini pamoja na Kingereza na Xosa ni wa mtindo anoueleza ni Afro Soul.

“Kwa vile ni mtindo wa Soul zaidi, hata hivyo ninachanganya na Jazz na R&B kwa sababu hiyo ni midundo niliyokulia nayo. Na mdundo wa Afro bila shaka unatokana na asili yangu na lugha za kiafrika."

Anasifu muziki wake kutokana na kupenda na kusikiliza wanamuziki wa Marekani na wale si muziki wa magwiji na mdundo wa Afrika Kusini kama kina Hugh Masekela au Miriam Makeba.

“Muziki wa Afrika Kusini ulikuwa uempigwa marufuku nilipokuwa ninakuwa. Kwa hivyo sikuwa ninamsikiliza Miriam kwa mfano, hadi baadae kwa hivyo nyimbo nyingi tulokuwa tunasikiliza ni wa kina Stevie wonder, Aretha Franklin na wengine.”

Akiwa tayari ni mashuhuru huko Afrika Kusini Lira hivi sasa anasema yuko tayari kushuka kwenye jukwa la kimataifa. Tayari hapa marekani alishatembelea mwaka 2011 akifanya ziara ya majimbo matano mbele ya maelfu ya mashabiki. Anasema anawakilisha vijana wa afrika Kusini ambao wananufaika na mipaka iliyofunguliwa ambayo hapo awali ilikuwa imebanwa au kufungwa kabisa.

“Changamoto tuliyokuwa nayo katika kizazi hichi chetu , ambacho hivi sasa kiko huru, ni tufanyeje na uhuru huu wetu, Tufanye nini, inamaana gani kwangu mimi, kwangu mimi inamaana nina uhuru wa kufuata ndoto yangu nan a kuipanga ninapoendelea mbele. Hivi sasa kwa vile nimeshaikomboa afrika ninapanua nafasai zangu hivyo ndivyo ninavyo tumia uhuru wangu."
Lira akiimba mjini Washington
Lira akiimba mjini Washington


Akidhamiria kuendeleza utamaduni wake, Lira anasema kama wengine wa kizazi chake anajichukulia kama kiungo cha kuleta mabadiliko, kwa kuleta amani na umoja duniani kupitia muziki.

“Ninajitambulisha kama mwafrika wa mjini, yani tulicho nayo kama waafrika ni kwa sehemu tunaurithi wetu, lakini tunahamu pia kuwa walimwengu tughangiye katika utandawazi. Kile ninachona mimi ni kwamba imani ya kiafrika inaweza kuisaidia dunia ili kurudi katika imani ya kibinadamu yani Ubuntu kama tunavyiosema huko afrika kusini.”
Lira hivi sasa anatayarisha album mpya.
XS
SM
MD
LG