Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Aprili 26, 2024 Local time: 13:50

Kenya Muslim Youth wanauhusiano na al-Shabab bado


Wapiganaji wa al-Shabab wakifanya mazowezi ya kijeshi kaskazini ya Mogadishu.
Wapiganaji wa al-Shabab wakifanya mazowezi ya kijeshi kaskazini ya Mogadishu.
Jopo la Umoja wa Mataifa la ufuatiliaji hali ya mambo Somalia na Eritrea linasema kundi moja la vijana wa kislamu nchini Kenya Muslim Youth Center kinachotuhumiwa kuwaandikisha wapiganaji kwa ajili ya kundi la kisomali la Alshabab kimebadili jina na kujipanga upya.

Kitu kimoja ambacho hakijabadilika na kundi hilo ni kwamba wanachama wake bado wana ushirikiano na al-Qaeda.

Ripoti mpya ya jopo la ufuatiliaji la Umoja wa Mataifa, iliyotolewa kwa siri mapema wiki hii, haitowi maelezo ya kutosha kuhusu shughuli za hivi karibuni za kundi hilo la vijana wa kislamu (MYC) . Hiyo ikilinganishwa na ripoti yake ya mwaka 2011 ambayo inaelezea kuhusika kwa kundi hilo katika kuwaandikisha na kuchangisha fedha kwa ajili ya kundi la al-Shabab.

Kufuatia ripoti hiyo, kundi moja la wakazi katika mtaa wa Majengo mjini Nairobi, walikwenda mahakamani kutetea hoja kuhusiana na ushawishi wa MYC katika msikiti mmjoa wa mtaa huo unaojulikana kama Pumwani Riyadha.

Mahfoodh Awadhi, kiongozi wa vijana wa Majengo na mwenyekiti wa baraza la kitaifa kuhamasisha masuala ya kiislam anasema jumuiya yake ilishangazwa wakati mahakama iliporuhusu kamati yenye uhusiano na MYC kuendelea kuusimamia msikiti ukichukulia shutuma dhidi yake za kushirikiana na wanamgambo.

“Kulikuwa na amri mbili za mahakama ambazo ziliwazuia kusimamia msikiti . Na baadaye jaji mwingine alichukua kesi na kutoa amri kwamba ni sharti kwa msajili wa vyama kulitambua kundi hilo. Walitajwa kwa makosa kuwa wanaandikisha wanamharakati na kuunga mkono Al-Shabab.”

Mahakama ilitoa amri kwa kamati ya msikiti wa Riyadh kuchagua uongozi mpya na kwa msajili wa vyama wa Kenya kusimamia uchaguzi huo.
Lakini nyaraka zilizopatikana na VOA kutoka kwa msajili zinaonyesha kwamba msikiti huo badala yake ulibadilisha uongozi wa sasa na kuteuwa wanachama wapya watatu tu kutoka kwenye bodi ya wanachama 17.

Mmoja wapo wa wanachama hao wapya ni Hadija Nduta Njuguna ambaye ameteuliwa kama naibu katibu mpya na mwanamke pekee kwenye bodi hiyo.
Kwa mujibu wa vyanzo mbali mbali Njuguna ni mke wa zamani wa Ahmed Iman Ali katibu aliyemtangulia wa kamati hiyo ambaye alitajwa katika ripoti ya Umoja wa Mataifa ya 2011 kwa kuongoza wapiganaji wa al-shabab Somalia.

Mwanachama mwingine ambaye anayetajwa kama mfadhili wa kamati ya msikiti ni Mohamed Mwai Abbas aliyeshukiwa kuwa amefanya mafunzo ya mapigano na al-Shabab huko Somalia.

Kiongozi wa chama cha wanasheria wa Kenya, Law Socitey, Apollo Mboya amesema kunahitaji kuwepo na ukaguzi wa dhati kabla ya kuandikisha makundi au vyama vyenye kutiliwa shaka.

“Tunahitaji mabadiliko makubwa katika jinsi tunavyofanya kazi, utaratibu wetu wa kuandikisha watu, kusajili makundi. Hii si enzi ambayo mtu anaweza tu kuleta nyaraka ukafikisha mezani na utaraji walioko kwenye meza wataziwasilisha kwenya idara ya ujasusi ukiwa namatumaini idara ya ujasusi itaeleza huyu mtu ni nani."

Ingawa Mboya anasema mabadiliko yanahitajika, anakubali kwamba kupata ushahidi kuthibitisha ugaidi na kufungua mashitaka ni ngumu. Kwa sababu ya hilo anasema wakenya wasikosowe mahakama kwa kuwaachia watu wanaoshukiwa kuwa magaidi au kuwa na uhusiano na shughuli za kiaidi.

“Sasa wakati mahakama haipewi maelezo ya kutosha kuhusiana na jambo Fulani, basi mahakama itaamua kufuatana na kilichopo mbele yake, hatuwezi kuendelea kutoa uvumi na ndio maana nasema tena inahusiana na kukusanya taarifa za ujasusi, inahusiana na kufanya kazi kwa pamoja idara mbali mbali za serikali. Je taarifa za kijasusi zinatumiwa kwa pamoja na Polisi na waendesha mashtaka?”

Kundi la Muslim Youth Center kilianzishwa Desemba 2008, kama kundi lenye lengo la kuwawezesha vijana na kuendeleza amani. Lakini katika vitendo, kundi hilo limejihusisha katika kuwaandikisha vijana wa Kenya kwenda kupambana bega kwa bega na al-Shabab na baadhi ya wanachama wametamba wazi wazi kuwa na uhusiano na al-Qaida.
XS
SM
MD
LG