Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Aprili 26, 2024 Local time: 13:37

Al-Shabab waua abiria 28 kaskazini mashariki mwa Kenya


Wanamgambo wa al-Shabab
Wanamgambo wa al-Shabab

Polisi kaskazini mashariki mwa Kenya wanasema watu waliokuwa na bunduki wanachama wa kundi la Al-Shabab wamevamia basi moja na kuua abiria 28 ambao si waislamu ambao walichaguliwa kutokana na abiria 60 waliokuwa ndani ya basi hilo.

Kundi la wanamgambo wa kisomali la Al-Shabab wamedai kuhusika na shambulizi, likisema ni majibu kwa uvamizi wa karibuni wa majeshi ya usalama ya Kenya uliofanywa katika misikiti mjini Mombasa.

Maafisa wanasema wanamgambo walilikamata basi hilo Jumamosi kiasi cha kilometa 50 kutoka mji wa Mandera karibu na mpaka wa Kenya na Somalia.

Kenya imekumbwa na mlolongo wa mashambulizi ya silaha na mabomu ambayo yanadaiwa kufanywa na wanamgambo wa Al-Shabab wenye uhusiano na Al-Qaida tangu Kenya ipeleke majeshi yake nchini Somalia mwaka 2011.

Wanajeshi wa Kenya ni sehemu ya tume ya ulinzi wa amani ya Umoja wa Afrika nchini Somalia ambayo inaisaidia serikali dhaifu ya Somalia ambayo inaungwa mkono na Umoja wa mataifa ili kupambana na uasi wa Al-Shabab nchini humo.

XS
SM
MD
LG