Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Aprili 26, 2024 Local time: 14:12

Huduma ya UBER yakosolewa barani Afrika


Dereva na abiria wa Uber nchini Afrika kusini
Dereva na abiria wa Uber nchini Afrika kusini

Huduma mpya ya usafiri wa taxi ijulikanao kama UBER inajaribu kuondoa asili ya huduma ya taxi barani Afrika lakini kampuni hiyo ya UBER yenye makao yake Marekani inatakiwa kukubali tamaduni za kiafrika, pamoja na kujirudisha nyuma kutoka kwenye utamaduni asilia ya taxi.

UBER ambayo huduma yake inapatikana kiurahisi kwa njia ya simu ya mkononi kwanza ilijitangaza yenyewe nchini Afrika kusini mwaka 2013 na hivi sasa inapatikana katika miji ya Cape Town, Johannesburg, Port Elizabeth na Durban. Huku ikiwasilisha changamoto za kuunda utamaduni zaidi wa usafiri wa umma, pia inatoa ajira mpya katika soko mahala ambapo ajira zilikuwa hafifu.

Huduma hii ya UBER ilianzishwa Nigeria mwaka uliofuata na huduma zinapatikana mjini Lagos na Abuja. Ilipofika mwaka 2015 huduma hii ilikuwepo pia mjini Mombasa nchini Kenya.

XS
SM
MD
LG