Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Aprili 28, 2024 Local time: 16:59

Blinken atahadharisha hatari za kuwepo habari potofu na za uongo uchaguzi wa 2024


Antony Blinken
Antony Blinken

Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken amesema mwaka 2024 ni mwaka wa uchaguzi usio wa kawaida wa kuangazia hatari kwa habari potofu na  za uongo katika mitandao kwenye Mkutano wa demekrasia unaofanyika mjini Seoul leo.

Blinken ambaye anahudhuria Mkutano wa tatu wa demokrasia, alirudia shutuma za Washington kwamba Russia na China zinahusika na kampeni za kimataifa zinazolenga kubadilisha habari.

Baadhi ya maafisa wa Ulaya pia wameishutumu Russia kwa kufanya kampeni za upotoshaji wa kutumia AI.

Rais wa Russia Vladimir Putin
Rais wa Russia Vladimir Putin

Vitisho vya kidijitali kwa demokrasia na jinsi teknolojia inavyoweza kukuza demokrasia na haki za binadamu kwa wote, vinatarajiwa kuwa katika agenda kuu ya mikutano ya siku tatu inayohudhuriwa na wawakilishi kutoka zaidi ya nchi 30, kuanzia Costa Rica hadi Marekani na Ghana.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken anaeleza: “Mwaka jana mwezi Septemba tulitoa ripoti iliyoeleza kwa kina jinsi China ilivyowekeza mabilioni ya dola kwa ajili ya kueneza propaganda na kubadilisha mazingira ya taarifa kote ulimwenguni.

Rais wa China Xi JInping
Rais wa China Xi JInping

Kwa mfano kununua king’amuzi cha televisheni Afrika na kutojumuisha chaneli za habari za kimataifa kutoka kwenye vifurushi vya usajili au kutumia kampuni tanzu za ndani ili kununua kwa siri makampuni ya vyombo vya habari kusini mashariki mwa Asia ambayo yanaendesha habari za watu wa Jamhuri ya watu wa China."

Forum

XS
SM
MD
LG