Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Mei 17, 2024 Local time: 11:00

Viongozi wa dunia wakubali kushirikiana ili kukabiliana na athari zisizotarajiwa za teknolojia ya AI


Viongozi walohudhuria mkutano wa AI Uingereza
Viongozi walohudhuria mkutano wa AI Uingereza

Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres ametoa wito wa kubuniwa mkakati wa kimataifa, wa pamoja na endelevu ili kukabiliana na hatari zinazotokana na maendeleo ya kasi ya teknolojia ya komputa ya AI.

Guterres alitoa wito huo wakati wa mkutano wa siku mbili nchini Uingereza akisisitiza juu ya haja ya kupatikana suluhisho mpya ili kupunguza mwana uliyopo kati ya AI na usimamizi wake.

Amependekeza kwamba ni lazima suluhu hiyo iwe chini ya misingi ya katiba ya Umoja wa Mataifa na tangazo la kimataifa la Haki za Binadam.

Mkutano huo wa kwanza wa aina yake ulifanyika katika jengo la Bletchley Park na kuhudhuriwa na viongozi wa kisiasa kutoka mataifa 28 wakiwemo Waziri Mkuu wa Uingereza Rishi Sunak, Makamu Rais wa Marekani Kamala Harris na Mkuu wa Umoja wa Ulaya Ursala von der Leyen.

Delegates sit at a roundtable during a plenary session during the UK Artificial Intelligence (AI) Safety Summit at Bletchley Park, in central England, on November 2, 2023.
Wajumbe kwenye meza ya duara wakati wa mkutano wa kilele wa teknolojia ya AI kwenye jengo la Bletchley Park Uingereza

Baadhi ya viongozi wamesema kanuni na masharti ya haraka sio njia bora kuendelea mbele na baadhi ya makampuni ya teknolojia ya AI wanahofia kwamba kuwekwa kanuni na masharti ya usimamizi huwendea kukapunguza kasi za maendeleo ya teknolojia hiyo kabla haijafika kilele cha uwezo wake.

Hata hivyo Katibu Mkuu Guterres ametoa wito kwa wabunge na wasimamizi kuchukua hatua za kuwa mbele ya wimbi la AI badala ya kulazimika kufuata nyuma.

Kwenye mkutano na waandishi habari baada ya mkutano huo waziri mkuu Sunak alitangaza makubaliano mengine ya kihistoria ambapo mataifa yameahidi kufanya kazi pamoja katika kufanya majaribio ya usalama ya vifaa vipya vya AI kabla ya kutolewa.

Kuna mipango ya kufanya mikutano mingine huko Korea Kusini na Ufaransa katika mwaka unaokuja.

Forum

XS
SM
MD
LG