Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Aprili 26, 2024 Local time: 09:16

Idara za usalama Burundi zashutumiwa na Amnesty kuwatesa wapinzani


Polisi wa Burundi wakimkamata muandamanaji. katika mji mkuu Bujumbura, Burundi, Mei 29, 2015.
Polisi wa Burundi wakimkamata muandamanaji. katika mji mkuu Bujumbura, Burundi, Mei 29, 2015.

Shirika la Amnesty international limeshutumu idara za usalama za Burundi kwa kuwakamata waandamanaji wanaopinga serikali na kuwapiga ili kuwashurutisha wakiri makosa na kunyamazisha upinzani.

Maafisa wa nchi hiyo wanashutumiwa kuhusika na vitendo vya utesaji na unyanyasaji dhidi ya watu waliokamatwa baada ya maandamano kuzuka mwezi Aprili huko Burundi katika ripoti iliyoitwa “Niambie nini cha kukiri” . Wakati rais Nkurunzinza alipotangaza kugombea kwa muhula wa tatu na kuwakasirisha wapinzani waliosema kuwa alikuwa akikikiuka ukomo wa madaraka uliowekwa kwa mujibu wa katiba.

Mkurugenzi wa kanda wa Amnesty International Sarah Jackson aliorodhesha baadhi ya shutuma hizo.

XS
SM
MD
LG