Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Mei 09, 2024 Local time: 01:09

Wamarekani washiriki katika uchaguzi wa kati kati ya muhula


Mabango ya wagombea yakionekana kwenye baadhi ya vituo vya kupiga kura Marekani
Mabango ya wagombea yakionekana kwenye baadhi ya vituo vya kupiga kura Marekani

Wapiga kura kote Marekani wameanza kupiga kura katika uchaguzi wa kati kati ya muhula ambao utaamua kama wa-Democrat au wa-Republican wanadhibiti baraza la seneti katika muda wa miaka miwili uliobaki madarakani kwa Rais Barack Obama.

Viti vyote 435 katika baraza la wawakilishi na theluthi moja ya viti 100 vya baraza la seneti vinagombaniwa. Lengo kuu ni baraza la seneti, ambapo wachambuzi wengi wa kisiasa wanasema wa-Republican wanaelekea kushinda viti sita muhimu ili kuweza kudhibiti baraza hilo kutoka chama cha Democrat cha bwana Obama ambacho kinashikilia wingi wa viti 55.

Huku kiwango cha utendaji kazi cha rais kikiwa kimeshuka mpaka asilimia 40 fursa nzuri ya chama cha Republican ni viti kadhaa ambavyo bwana Obama alivipoteza miaka miwili iliyopita wakati wa kampeni yake ya kuchaguliwa tena.

Wa-Republican wanatarajia kuendelea kushikilia na pengine kujiongezea viti zaidi katika bunge.

Ukusanyaji maoni wa hivi karibuni unaonyesha kwamba wagombea wa chama cha Republican watashinda kirahisi katika kinyang’anyiro cha seneti huko West Virginia, South Dakota na Montana majimbo ambayo hivi sasa yanashikiliwa na wa-Democrat. Maoni hayo pia yanaonyesha kuwa wa-Republican pia wanatarajiwa kushinda kinyang’anyiro cha seneti katika majimbo ya Iowa, Colorado na Alaska japokuwa huenda ikachukua saa kadhaa au hata siku kabla ya matokeo rasmi kujulikana.

Vinyang’anyiro viwili huko kusini, Georgia na Louisiana wamefungana na watahitajika kufanya uchaguzi wa marudio.

XS
SM
MD
LG