Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Aprili 27, 2024 Local time: 07:23

Misaada ya kimataifa yaanza kuwasili Phillippines.


Wakazi waliookolewa wakijiandaa kupanda ndege ya kijeshi ya Marekani katika uwanja wa ndege wa Tacloban huko Philippines November 13, 2013.
Wakazi waliookolewa wakijiandaa kupanda ndege ya kijeshi ya Marekani katika uwanja wa ndege wa Tacloban huko Philippines November 13, 2013.
Msaada wa dharura wa kimataifa umeanza kuwasili kwa wingi huko Philipines, lakini maelfu na maelfu ya watu wangali wana mahitaji makubwa ya chakula na hifadhi siku tano baada ya kupoteza makazi yao kutokana na kimbunga kikali cha Haiyan.

Katika ishara ya watu kukata tamaa watu wanane waliuwawa Jumatano pale ukuta wa ghala la serikali lenye mchele ulipoanguka wakati walionusurika walipovamia .

Wakati huo huo Manowari ya kivita ya Marekani USS George Washington iliwasili Jumatano katika kisiwa kilichoharibiwa vibaya sana na kimbunga Haiyan ili kusaidia watu wengi ambao wamebaki wakiwa na mahitaji makubwa ya chakula na huduma nyingine muhimu.

Meli hiyo ya kivita inasaidia kuharakisha mahitaji ya dharura katika mji wa Tacloban ambao ulikuwa karibu uharibiwe kabisa Ijumaa na moja ya vimbunga vikubwa kuliko vyote kuwahi kurekodiwa.

Meli hiyo ni sehemu ya kikosi cha meli ambazo zitatoa mamilioni ya lita za maji ya kunywa kila siku. Pia inabeba helikopta na ndege nyingine maalum zinazohitajika ili kupeleka vifaa vya kuokoa maisha katika maeneo ya ndani sana.
XS
SM
MD
LG