Bwana Obama aliapishwa kisheria Jumapili ikulu kwa sababu katiba inataka rais kuapishwa Januari 20. Jaji mkuu John Roberts aliongoza taratibu za kuapishwa kwa rais kama alivyofanya mwaka 2009.
Bwana Obama alikula kiapo muda mfupi kabla ya saa sita mchana kwa saa za Washington DC, akiwa na mkewe Michelle Obama na wanawe Malia na Sasha.
Rais barack Obama anaapishwa Januari 21 kwa mhula wa pili akiwa Mmarekani wa kwanza mwenye asili ya kiafrika kuchaguliwa kwa mara ya pili.