Washirika wa Mugabe waandamana kupinga utawala wake

Wapiganaji wa zamani nchini Zimbabwe walimgeuka mshirika wao wa muda mrefu rais Robert Mugabe wakimuelezea kuwa ni dikteta katika kulaani juu ya kuchukua kwake madaraka na hasara inayoongezeka kutokana na matatizo ya kiuchumi.

Wapiganaji hao wa zamani ambao wamemfanyia kampeni mara nyingi kwa ghasia tangu mwaka 2000 wamesema wanaondoa uungaji wao mkono wa kisiasa taarifa ambayo imeweka tofauti katika kiini cha wenye mamlaka Zimabawe.

Uongozi wa Mugabe umeshindwa kudhibiti rushwa iliyokithiri na kutosimamia vizuri uchumi na kupelekea kuzorota kwa uchumi wa taifa ambapo athari zake zinaonekana nchi nzima chama cha wapiganaji hao wa zamani ZNLVA kilieleza.