Ziara ya Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani nchini Kenya

Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken akipanda ndege Uwanja wa Ndege wa Kikosi cha Anga Andrews, Maryland, Nov. 16, 2021. Akianza ziara yake itakayo mchukua siku tano akizuru Kenya, Nigeria, na Senegal.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken akihutubia katika Ubalozi wa Marekani mjini Nairobi, Kenya Novemba 18, 2021. Andrew Harnik/Pool via REUTERS

Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken akiwasili kufanya mkutano na Katibu Mtendaji wa Mamlaka ya Kiserikali kuhusu Maendeleo (IGAD) Workneh Gebeyehu (hayuko pichani) , katika Hoteli ya Sankara Nairobi, Kenya, Novemba 17, 2021. Blinken akiwa anajitayarisha kuelekea Nigeria katika ziara yake nyingine.​(Photo by Andrew Harnik / POOL / AFP)

Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken akisaini kitabu cha maombolezo katika Kumbukumbu ya August 7, Nairobi, Kenya, Jumatano, Nov. 17, 2021, ikiwa ni eneo mojawapo la shambulizi la mabomu katika ubalozi wa Marekani mwaka 1998 lililoua mamia ya watu katika miji mikuu miwili ya Afrika Mashariki​. Blinken alikuwa katika ziara ya siku tano nchini Kenya, Nigeria, na Senegal. (AP Photo/Andrew Harnik, Pool)

Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken akionyesha kitu huku Waziri wa Mambo ya Nje wa Kenya Balozi Raychelle Omamo akiangalia Jengo la Wizara ya Mambo ya Nje la Marekani jijini Washington, DC, Julai 16, 2021. (Photo by TOM BRENNER / POOL / AFP)

Waziri wa Mambo ya Nje Antony Blinken akiongea akiwa na Waziri wa Mambo ya Nje wa Kenyah Raychelle Omamo katika mkutano na waandishi wa habari Hoteli ya Serena, Nairobi, Kenya, Nov. 17, 2021.

Waziri wa Mambo ya Nje Antony Blinken akizungumza katika mkutano wa pamoja wa jumuiya ya kiraya Hoteli ya Sankara, Nairobi, Kenya, Jumatano, Nov. 17, 2021.

Blinken and Raychelle Omamo
Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken (Kushoto) akiwa na  Waziri wa Mambo ya Nje wa Kenya Raychelle Omamo (R) akizungumza katika mkutano wa waandishi wa habari Hoteli ya Serena, Nairobi, Kenya, on Novemba 17, 2021. (Photo by Simon MAINA / AFP)

Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, Antony Blinken anaendelea na ziara yake ya mataifa matatu akiwa tayari nchini Nigeria. Ziara yake itakayo chukua siku tano akiwa tayari amezuru Kenya, na anatarajiwa kumalizia na Senegal.