Wakenya milioni 28 kwenye hatari ya Malaria

Mtoto apatiwa chanjo ya Malaria katika eneo la Kilifi, Kenya.

Jumla ya wakenya milioni 28 wako katika hatari ya kuambukizwa ugonjwa wa Malaria nchini Kenya huku wakihimizwa kulala ndani ya neti zilizotibiwa ili kujikinga mbu. Kufuatia viwango vya juu vya ugonjwa wa Malaria nchini humo hasa katika eneo la Pwani ambako maadhimisho ya kitaifa yamefanyika Jumatatu

Your browser doesn’t support HTML5

Malaria Kenya


Akizungumza kwenye sherehe za maadhimisho hayo, kaimu mkurugenzi wa afya nchini Kenya, Jackson Kioko, amekariri kuwa japo kuna hatua ambazo zimepigwa katika vita dhidi ya Malaria katika kipindi cha miaka kumi iliyopita, jumla ya visa milioni 8 vya ugonjwa huo viliripotiwa mwaka uliopita. Amina Chombo anaeleza zaidi. Sikiliza taarifa kamili.