Waziri wa Marekani aendelea na ziara yake Kenya

Waziri wa maswala ya ndani wa Marekani, Sally Jewel ameendelea na ziara yake nchini Kenya kuangazia tatizo la uwindaji haramu.

Ziara yake Bi Jewell vilevile inahusu biashara ya bidhaa zinazotokana uwindaji haramu ambapo alizuru bandari kuu ya Kenya mjini Mombasa.

Katika ziara hiyo Jewell amesisitiza azma ya Marekani kushirkiana na Kenya na mataifa ya Afrika Mashariki kukabiliana na uovu huo.

Eneo la Afrika Mashariki limekumbwa sana tatizo la uwindaji haramu wa Tembo ya Vifaru kitu ambacho kinatishia kutoweka kwa wanyama hao wa urithi wa taifa.

Your browser doesn’t support HTML5

Ripoti ya mwandishi wetu Liberty Adede ya ziara ya waziri wa Marekani kuhusu ujangili