Watu tisa wakamatwa kuhusiana na mlipuko wa bomu Arusha

Waathiriwa wa shambulio la bomu kwenye kanisa la St. Joseph Mfanyakazi karibu na Arusha

Maafisa wa serikali ya Tanzania wanasema wamewakamata washukiwa tisa kwa shutuma za mlipuko wa bomu uliotokea kwenye kanisa moja mjini Arusha siku ya Jumapili.

Sauti ya Amerika-VOA ilizungumza kwa njia ya simu na mkuu wa mkoa wa Arusha bwana Magesa Mulongo juu ya watu waliokamatwa ambapo alisema raia hao wa kigeni walikamatwa wakijaribu kuvuka mpaka kuingia nchini Kenya.

Your browser doesn’t support HTML5

Mahojiano na mkuu wa mkoa wa Arusha, Magesa Mulongo


Maafisa nchini humo wanasema raia watatu wanatoka umoja wa falme za kiarabu-UAE na sio Saudi Arabia kama ilivyoripotiwa awali. Wizara ya mambo ya nje ya UAE ilithibitisha kwamba raia wake watatu walikamatwa nchini Tanzania na ilisema inafuatilia maendeleo ya uchunguzi huo.