Watetezi wa vyombo vya habari wanaikosoa Misri kwa ukandamizaji wake kwa waandishi wa habari kufuatia kukamatwa kwa mchora katuni na mwandishi wa habari.
Serikali ya Misri iliwakamata waandishi wa habari kama sehemu ya ukandamizaji mkubwa ukiwa ni kama kujibu wito wa maandamano dhidi ya Rais Abdel Fattah el-Sissi, kwa jinsi anavyoshughulikia uchumi.
Maandamano hayo hayakufanyika, lakini serikali iliwakamata takriban watu 125, wakiwemo Khaled Mamdouh na Ashraf Omar.
Wote wawili walishikiliwa bila mawasiliano kwa siku kadhaa.
Waandishi wa habari kadhaa walikusanyika katika makao makuu ya Shirika la Waandishi wa Habari la Misri katikati mwa jiji la Cairo wiki iliyopita kupinga kukamatwa na kuonyesha mshikamano na wenzao waliofungwa jela, Yeganeh Rezaian ameiambia VOA.
Yeye ni mratibu wa muda wa Mashariki ya Kati na Afrika Kaskazini katika Kamati ya Kulinda Wanahabari, CPJ.