Warundi wauanza mwezi wa Ramadhani kwa khofu ya usalama na sukari

Baadhi ya waumini wa kiislam nchini Burundi

Waumini wa dini ya kiislamu nchini Burundi wameungana na waislam wengine ulimwenguni kuanza funga ya mwezi mtukufu wa Ramadhan jumatatu hii.

Lakini waumini hao wana wasi wasi kuhusu usalama wao hasa wakati wa sala za usiku katika nchi hiyo inayokabiliwa hii sasa na mgogoro wa kisiasa.

Mbali na usalama, bidhaa kama vile sukari inayotegemewa sana wakati wa chakula cha jioni cha futari ambapo bidhaa hiyo imeanza kukosekama na kutoa changamoto kubwa katika kufanikisha funga za waumini hao ambayo ni nguzo mojawapo kati ya nguzo tano muhimu katika dini ya kiislamu.

Mwandishi wetu wa Bujumbura Haidallah Hakizimana ametutumia taarifa ifuatayo.

Your browser doesn’t support HTML5

Ripoti ya Haidallah Hakizimana wa Bujumbura, Burundi