Wananchi wa DRC waiomba MONUSCO kuongeza juhudi zao za ulinzi

Wanajeshi wa MONUSCO kwenye kituo cha ukaguzi huko DRC

Siku chache baada ya baraza la usalama la Umoja wa Mataifa kuongeza muda kwa kikosi cha jeshi la Umoja wa mataifa- MONUSCO huko Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo- DRC, sasa mashirika ya kiraia na yale ya kutetea haki za binadamu huko Congo Kinshasa wakiwemo wananchi wanakiomba kikosi cha MONUSCO kuhakikisha mwaka huu wahakikisha amani inapatika mashariki mwa Congo.

Mashirika hayo pamoja na wananchi wametoa wito huo kwa Umoja wa mataifa kuonesha nguvu zake na kuyashughulikia ipasavyo matatizo ya wapiganaji wa makundi ya pande zote katika eneo hilo.

Mwandishi wetu wa Sauti ya Amerika-VOA, Austere Malivika anaripoti zaidi kutoka Goma, DRC.

Your browser doesn’t support HTML5

Ripoti ya Austere Malivika kutoka Goma huko DRC