Wanajeshi wa Somalia watawanywa katika vikosi vingine

Serikali ya Somalia imekiri kwamba usambazaji wa mgao  kwa wanajeshi wake wasomi waliopata mafunzo Marekani umepelekwa kwingine ndai ya vitengo vyake ya jeshi. 

Katika taarifa iliyotolewa jana jioni, serikali imesema imefanya uchunguzi ambao umesababisha kusimamishwa kazi na kuzuiliwa kwa maafisa.

Idadi na utambulisho wa maafisa waliosimamishwa na wanaozuiliwa bado haijawekwa wazi.

“Jeshi la Taifa la Somalia katika miaka michache iliyopita limeboresha juhudi zake za uwajibikaji kulingana na ajenda yake ya mageuzi,” taarifa hiyo ilieleza.

“Wakati wa uchunguzi huo Vikosi vya Kitaifa vya Majeshi ya Somalia vimeripoti kubadilishwa kwa mgao wa Danab ndani ya kitengo cha vikosi vyake.

Serikali ya Shirikisho ya Somalia, inachukulia matukio haya kwa uzito na imeanzisha uchunguzi mara moja.