Wanaharakati waelezea imani na utawala wa Magufuli

Waziri Mkuu wa Tanzania, Kassim Majaliwa

Serikali ya mpya ya Tanzania chini ya Rais John Magufuli imechukua hatua kadha zinazo onyesha nia ya kutekeleza ahadi ya kupambana na rushwa nchini humo.

Viongozi wa juu katika utawala wa Rais Magufuli wamekuwa wakifanya ziara za kushtukiza katika baadhi ya maeneo makubwa yanayotoa huduma za umma, ikiwa ni pamoja na ziara ya pili Alhamis ya Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, katika bandari ya Dar Es Salaam ili kujionea utendaji wa kazi katika bandari hiyo.

Your browser doesn’t support HTML5

Mahojiano ya VOA na mwanaharakati Fadhili Bwagalilo

Sauti ya Amerika-VOA-ilizungumza na mwanaharakati wa maendeleo ya jamii nchini Tanzania, Fadhili Bwagalilo, na kumuuliza kwanza endapo anadhani juhudi hizi zitakuwa endelevu au zitaishia njiani.

Bandari ya Dar-es-Salaam, Tanzania

Watanzania kwa asilimia kubwa wanaunga mkono juhudi za uongozi wa Rais John Magufuli alizoanza nazo katika kudhibiti matumizi yasiyokuwa ya lazima kwa serikali na vile vile katika juhudi ya kupambana na wakwepaji kodi pamoja na rushwa miongoni mwa taasisi za serikali.