Wafanyakazi wa serikali wadadisi amri ya kutoa maelezo ya kabila na dini

Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Emmanuel Tutubammanuel Tutuba

Serikali ya Tanzania imesema hakuna nia mbaya katika kuwataka wafanyakazi wa serikali kujaza upya wasifu wao na kuongeza maelezo juu ya kabila na dini zao, hatua ambayo ilisababisha kero huku wafanyakazi wakihoji busara ya agizo hilo jipya.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Emmanuel Tutuba alisema maelezo yanayotakiwa katika kujaza wasifu mpya ni kawaida kwa mfanyakazi na wale wanaopinga uamuzi huo wamekuwa na tafsiri potofu.

Maelezo hayo yataiwezesha mamlaka husika kujua taarifa binafsi za wafanyakazi zinapohitajika, amesema.

“Tumekuwa tukipendekeza majina ya baadhi ya watu katika taasisi mbalimbali… na halafu unaulizwa kuhusu taarifa binafsi za mtu huyu [lakini] maelezo kamili yanakosekana katika waraka wa wasifu wake wa awali,” amesema Tutuba.

“Watu wanaofanya uchunguzi wanataka kujua asili yako; uaminifu wako; iwapo wewe kweli ni Mtanzania; unatangamana vipi na watu wengine… Hili ni jambo la kawaida.”

Baraza la Wanazuoni wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (Udasa) na baadhi ya wafanyakazi wa Chuo Kikuu cha Dodoma wamekosoa matakwa ya baadhi ya taarifa hizo zinazotakiwa na serikali.