Wademokrat wachukua hatua juu ya ripoti ya Robert Mueller

Mwenyekiti wa kamati ya sheria ya bunge Jerry Nadler akizunguma na waandishi wa habari.

Mwanasheria Mkuu William Bar alitangaza atatoa ripoti kamili baada ya mambo ya siri kuondolewa

Wademokrat wengi wiki hii kutoka baraza la wawakilishi Marekani wameamua wiki hii kuchukua hatua ya kutumia hati ya mahakama kupata ripoti kamili ya mwendesha mashitaka maalum Robert Mueller juu ya uchunguzi wa Russia kuingilia kati uchaguzi wa Marekani wa mwaka 2016 na maafisa wa zamani watano wa White house.

Kamati maalum ya sheria imetaka kutolewa ripoti yote ifikapo Jumanne ya karibu kurasa 400 na ushahidi uliopo . Tangu mwanasheria Mkuu William Bar aseme wiki iliyopita kwamba atatoa ripoti kamili ifikapo kati kati ya Aprili kama si kabla ya hapo baada ya mambo ya siri kuondolewa.

Ikiwa siku ya mwisho ya jumanne imefika na ikaonekana haitawezekana kutimizwa kwa ahadi hiyo jopo la wabunge hao linapanga kupiga kura kuruhusu hati ya mahakama Jumatano na kumruhusu mwenyekiti wa kamati hiyo Jerrold Nadler kuamua vile anavyoona yeye kuwa inafaa.

Imetayarishwa na Sunday Shomari.