Wachezaji wa kimataifa wa kandanda wanaogua COVID-19

Zlatan Ibrahimovic wa AC Milan akishangilia goli alilofunga dhidi ya Bologna wakati wa michuano ya kundi A kati ya AC Milan na Bologna katika uwanja wa San Siro, mjini Milan, Italy, Jumatatu, Septemba 21, 2020.(AP Photo/Antonio Calanni)

Mshambuliaji wa timu ya AC Millan Zlatan Ibrahimovic aliambukizwa na virusi vya corona mwezi Septemba akisema,"COVID ilithubutu kumletea changamoto. Wazo baya." Alipona kutokana na maambukizo hayo wakati muda umefika wa pambano la Inter Milan huko Derby della Madonnia Oktoba 17.

Mchezaji bora wa dunia kwa miaka mitano Ronaldo akichezea timu yake iliyotoka sare 0-0 katika mchuano na Ufaransa wakati wa ligi ya Mataifa.

Cristiano Ronaldo, Juventus - Mshambuliaji - upande wa kushoto
Cristiano Ronaldo, mmoja wa nyota wakubwa wa kandanda duniani na ni miongoni mwa wanariadha maarufu zaidi, ameambukizwa virusi vya corona, Shirikisho la taifa la mpira wa miguu Ureno limetangaza Octoba 13. Mchezaji huyo mwenye umri wa maika 35 anaendelea vizuri na hana dalili za COVID-19 kwa mujibu wa Shrikisho hilo.
 

Kylian Mbappe wa Ufaransa akiutuliza mpira wakati wa mechi ya mpira wa miguu ya Ligi ya mataifa UEFA kati ya Croatia na Ufaransa kwenye uwanja wa Zagreb, Croatia, Jumatano, Octoba 14, 2020. (AP Photo/Darko Bandic)

Kylian Mbappe, PSG- Mshambuliaji - mfungaji magoli
Shirikisho la Mpira wa Miguu la Ufaransa (FFF) limethibitisha mapema Septemba Saint-Germain wa Paris na mshambuliaji wa Ufaransa Kylian Mbappe ameambukizwa COVID-19. Mbappe alitangaza kupona kwake na kurudu kucheza akifunga goli katika mchuano dhidi ya Nice wa mbao  3-0.

Neymar wa PSG wakati wa mchuano ya Ligi ya Ufaransa kati ya Paris Saint-Germain na Marseille katika uwanja wa Parc des Princes mjini Paris, Ufaransa, Jumapili, Septemba 13, 2020.(AP Photo/Michel Euler)

Mchezaji nyota wa kimataifa wa Brazil Neymar ni moja kati ya wachezaji kadhaa wa Paris Saint-Germain aliyeambukizwa COVID-19, kwa mujibu wa taarifa mbalimbali. Neymar alipona na yuko katika mafunzo na timu yake PSG kuanzia katikati ya mwezi Septemba.
 

Paulo Dybala wa Juvakishangilia baada ya kufunga goli wakati wa mechi ya Italian Serie A kati ya Genoa na Juventus katika uwanja wa Luigi Ferraris mjini Genoa, Itali, Jumanne, Juni 30, 2020.(Tano Pecoraro/LaPresse via AP)

Dybala ameambukizwa COVID-19 katikati ya janga la hili huko Itali, Dybala alianza mafunzo tena mwisho wa mwezi Machi baada ya kupona kutokana na maambukizi hayo
 

Callum Hudson-Odoi wa Chelsea wakati wa mechi ya Ligi ya Premier ya Uingereza kati ya Chelsea na Arsenal katika uwanja wa Stamford Bridge, London, Uingereza, Januari 21, 2020.(AP Photo/Leila Coker)

Mchezaji wa Chelsea Callum Hudson- Odoi ametangaza ameambukizwa na COVID-19.
Hudson-Odoi ni mchezaji wa mpira wa miguu wa kwanza katika Ligi ya Premier ya Uingereza kuthibitisha kuambukizwa. Winger huyo wa Chelsea 'amepona kabisa' kutokana na virusi vya corona mwisho wa mwezi Machi.
 


Paul Pogba, Manchester United - Midfielder

Midfielder wa Manchester United Paul Pogba ameondolewa kutoka katika kikosi cha Ufaransa kinachoshiriki Ligi ya Mataifa UEFA mwisho wa mwezi Agosti baada ya kuambukizwa virusi vya corona. Pogba amerejea kuendelea na mafunzo katika timu ya Manchester United katikati ya mwezi Septemba baada ya kutengwa.

Paul Pogba wa Manchester United akikimbia na mpira wakati wa mechi ya Ligi ya Premier ya Uingereza kati ya Manchester United na Tottenham Hotspur katika uwanja wa Old Trafford mjini Manchester, Uingereza, Jumapili Oktoba 4, 2020. (Carl Recine/Pool via AP)

Meneja wa Arsenal Mikel Arteta akitoa ishara pembeni ya uwanja kwa wachezaji wake wakati wa mechi ya Ligi ya Premier ya Uingereza kati ya Arsenal na Sheffield United katika Uwanja wa Emirates mjini London, Jumapili, Octoba 4, 2020. (AP Photo/Kirsty Wigglesworth)

Meneja wa Arsenal Mikel Arteta ameambukizwa na COVID-19 mwezi Machi 12, kulingana na tamko la rasmi la klabu hiyo kupitia tovuti yake. Amepona kikamilifu na amerejea katika shughuli za Ligi ya Premier.

Sadio Mane wa Liverpool akishangilia baada ya kufunga goli wakati wa mechi ya Ligi ya Premier ya Uingereza kati ya Chelsea na Liverpool katika Uwanja wa Stamford Bridge.(Michael Regan/Pool via AP, File)

Mchezaji wa mpira wa miguu wa Senegal ameambukizwa virusi vya corona mapema mwezi Oktoba katika michuano ya Ligi ya Premier ya Uingereza. Mane hivi karibuni alirejea katika mafunzo baada ya yeye mwenye kujitenga.

Mambukizo ya virusi vya corona yakiingia katika awamu ya pili kwenye nchi nyingi za dunia, kuna baadhi ya wachezaji mashuhuri wa kandanda wanaougua ugonjwa wa COVID-19 unaosababishwa na virusi hivyo.