Viongozi wa vyama vya siasa wameanza kampeni huko London.

Waziri Mkuu wa Uingereza, Rishi Sunak akiwa mjini London

Wapiga kura wataamua baada ya miaka 14 Chama cha Conservative cha Waziri Mkuu Rishi Sunak kitabaki madarakani au la.

Viongozi wa chama cha siasa nchini Uingereza wameingia mitaani Alhamisi katika msukumo wa kusaka kura, wakianza kampeni ya wiki sita kabla ya uchaguzi wa Julai 4.

Wapiga kura wataamua kama baada ya miaka 14, Chama cha Conservative cha Waziri Mkuu Rishi Sunak kitabaki madarakani au kitapoteza kiti kwenda kwa chama cha upinzani cha Labour.

Chama cha Labour kinasema Uingereza inahitaji mabadiliko.

“Tutakomesha machafuko,” alisema kiongozi wa chama cha Labour, Keir Starmer, mgombea anayeongoza kwa nafasi ya Waziri Mkuu. Anasema “Kama wa-Conservative watapata miaka mingine mitano, watajisikia haki ya kuendelea kuongoza kama walivyo. Hakuna kitakachobadilika.”

Sunak alipanga tarehe ya uchaguzi siku ya Jumatano katika tangazo la televisheni. Watu wengi wakiwemo wabunge wengine wa Conservative, wanatarajia Sunak atatangaza kushindwa uchaguzi.

Waziri Mkuu amesema yuko tayari kuchukua hatua za kijasiri.

Katika wakati usiokuwa na uhakika unahitaji hatua za kijasiri ili kuleta usalama, Sunak aliliambia shirika la habari la BBC. “Hicho ndicho nitakacholeta.”

Waziri Mkuu wa Uingereza, Rishi Sunak. April 22, 2024.

Wapinzani wanasema Sunak alipanga tarehe ya mapema kwa sababu ya wasiwasi kwamba sheria yake ya uhamiaji itafeli.

Sheria hiyo inaruhusu waomba hifadhi wanaowasili nchini Uingereza bila ruhusa, katika nchi ya tatu ambayo inaelezewa ni salama. Uingereza imewakamata wahamiaji kadhaa ambao hawakutajwa kwa ajili ya kupelekwa nchini Rwanda mwezi Julai.

Kama nitachaguliwa, tutafuta safari za ndege," Sunak aliiambia redio ya LBC siku ya Alhamisi.

Sunak anapanga kuitembelea England, Scotland, Wales na Ireland Kaskazini katika siku mbili za kwanza za kampeni yake.