Viongozi wa mapinduzi ya kijeshi wafunga mipaka Guinea Bissau

Askari wa Guinea Bissau wakiondoka kwenye mkutano na waandishi wa habari katika makao makuu kijeshi huko Bissau.

Msafara wa jumuiya ya uchumi Afrika magharibi waelekea Guinea Bissau na huku mipaka imetangazwa kufungwa .

Viongozi wa mapinduzi nchini Guinea Bissau ya wiki iliyopita wamefunga mipaka ya bahari na anga ya nchi hiyo huku kukiwa na ongezeko la msukumo kuwataka waachie madaraka.

Haijajulikana mara moja kama kufungwa huko kwa mipaka kulikotangazwa Jumatatu kutaathiri msafara kutoka nchi za jumuiya ya uchumi Afrika Magharibi Ecowas .

Kundi hilo linatarajiwa mjini Bissau kukutana na viongozi wa kijeshi ambao walichukua madaraka alhamisi , muda mfupi kabla ya kampeni ya urais kuanza kwa uchaguzi wa duru ya pili.