Viongozi wa Afrika wajadili Usalama DRC, Somalia, Sahel na sehemu nyingine za Afrika

Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Antony Blinken (katikati), waziri wa mambo ya nje wa DRC Christophe Lutundula (kushoto) ma waziri wa mambo ya nje wa Zambia Stanley Kakubo wakisaini makubaliano ya ushirikiano Dec 13,2022

Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Antony Blinken amesema kwamba Marekani inafurahishwa na juhudi zinazochukuliwa na rais wa Angola Joao Lourenco katika kutatua mgogoro wa Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo.

Waziri wa ulinzi wa Marekani Lloyd Austin amehudhuria mkutano huo uliofanyika pembeni mwa mkutano wa viongozi wa Afrika unaoendelea hapa Washington DC.

Kulingana na msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya Marekani Ned Price, Blinken, Lloyd na Lourenco wamejadiliana pia kuhusu ushirikiano wa kiuchumi na usalama nchini Angola, kabla ya Blinken kukutana na marais wa Niger, Somalia na Djibouti katika kikao kilichoangazia ziara maswala ya usalama.

Mkutano kati ya rais wa Niger Mohamed Bazoum, Hassan Sheikh Mohamud wa Somalia, Ismail Omar Guelleh, waziri wa mambo ya nje wa Marekani Antony Blinken na waziri wa ulinzi Lloyd Austin, vile vile umeangazia utawala bora, ukuaji wa uchumi, usalama na haki za kibinadamu.