Ukraine imetungua ndege tano za Russia zisizokuwa na rubani

Mfano wa Drone aina ya Shahed.

Russia ilitumia drone tatu za Shahed na nyingine mbili ambazo hazikufahamika aina yake kwenye shambulio hilo, taarifa ilisema.

Ukraine imetungua ndege zote tano zisizokuwa na rubani zilizorushwa na Russia wakati wa shambulizi la usiku kucha, jeshi la anga la nchi hiyo limesema leo Ijumaa. Vikosi vya Russia pia vilitumia makombora matatu ya masafa marefu aina ya Iskander-M wakati wa shambulio hilo, kulingana na taarifa ya jeshi la anga kwenye ujumbe wa mtandao wa Telegram.

Russia ilitumia drone tatu aina ya Shahed na nyingine mbili ambazo hazikufahamika aina yake kwenye shambulio hilo, taarifa ilisema. Shirika la habari la Reuters liliripoti kuwa Russia ilitumia Drone ambazo hazikutengenezwa kwa ustadi mkubwa katika baadhi ya mashambulizi yake dhidi ya Ukraine ili kujaribu kutambua ulinzi wa anga na kutumika kama kupoeza mwelekeo.

Magavana wa mikoa ya Kyiv na Kirovohrad waliripoti hakuna uharibifu au vifo kufuatia shambulio hilo. Ulinzi wa anga ulifanya kazi katika mji mkuu Kyiv usiku kucha na mamlaka ya mji haikuripoti uharibifu.