Wamiliki viwanda Uganda walalamikia Kenya kukataa bidhaa zao

Mji mkuu wa Kampala, Uganda.

Wamiliki viwanda nchini Uganda wamelalamikia nchi ya Kenya kwa kutoagiza bidhaa zao wakisema kuwa hawana sababu ya kubaki kwenye Jumuia ya Afrika Mashariki.

Muungano wa wamiliki viwanda nchini Uganda Ijumaa limewasilisha ombi kwa Bunge likitaka Uganda ianze mikakati ya kujiondoa kwenye muungano wa jumuia ya Afrika Mashariki kutokana na hatua ya Serikali ya Kenya ya kususia bidhaa kutoka Uganda.

Your browser doesn’t support HTML5

Viwanda Uganda

Wenye viwanda hao walisema mbele ya kamati ya Bunge kuwa hatua hiyo ya Kenya ianonesha wazi kuwa Umoja wa Afrika Mashariki hauheshimiwi na kwa hivyo hakuna sababu ya Uganda kubaki ndani yake.

Mwandishi wetu wa Kampala Kennes Bwire anaripoti. Bonyeza kwa taarifa zaidi.