Ufaransa kuchunguza wakwepa kodi wenye akaunti za nje

Ripoti ya ICIJ (The Panama Papers)

Rais wa Ufaransa amesema Jumatatu kwamba nchi yake itaanza uchunguzi maalum juu ya wakwepa kodi wa Ufaransa wanaotumia akaunti za nje ya nchi kuficha utajiri wao, kama ilivyobainika katika taarifa kubwa zilizovuja.

Timu ya waandishi wa kimataifa wakifanyia kazi nyaraka ambazo zimevuja kutoka taasisi ya kisheria ya Panama wamechapisha baadhi ya uchunguzi wao juu ya makubaliano ya kifedha ya matajiri na watu maarufu na walio na mahusiano makubwa ya kisiasa na baadhi ya voongozi wa baadhi ya nchi. Taarifa hizo zimejulikana kama Panama Papers.

Hollande inasema uchunguzi utafanyika, kesi zitafunguliwa na zitasikilizwa.

Chanzo kisichokujulikana kimetoa nyaraka milioni 11.5 kutoka Panama taasisi ya sheria ya Mossack Fonseca kwa taasisi ya kimataifa ya waandishi wa uchunguzi (ICIJ) yenye makao yake hapa Washington.