Uchumi wa Rwanda watarajiwa kuendelea kukua

Jiji la Kigali Rwanda

Uchumi wa Rwanda unatarajiwa kukua kwa asilimia 6.6 mwaka 2024, ikilinganishwa na mwaka huu ambapo umekuwa kwa asilimia 6.2, Waziri wa fedha na Gavana wa Benki kuu wameandika barua kwa Shirika la Kimataifa la Fedha Duniani- IMF.

Mwezi February, Waziri Uzzie Ndagijimana alibashiri ukuaji uchumi utaongezeka kwa asilimia 7.5 katika taifa hilo la Afrika mashariki kwa mwaka 2024 na 2025. Uchumi ulikuwa kwa silimia 8.2 mwaka 2022.

“tunaona ukuaji wa pole pole wa muda, unaosukumwa na sera kali za fedha zinazohitajika, “alisema hayo,” Ndagijimana na Gavana wa Benki kuu John Rwangombwa katika barua ya Novemba 29 iliyotangazwa kwa umma jumatatu jioni.

Mwezi Novemba benki kuu ya Rwanda ilishikilia kiwango chake kikuu cha ukopeshaji kwa asilimia 7.5 ikisema iliona mfumuko wa bei ukishuka hadi kufikia kiwango cha asilimia 2 hadi 8 ifikapo mwishoni mwa mwaka.

Hata hivyo Ndagijimana na Rwangombwa wamesema mambo ya nje yanaweza kuchochea matarajio ya ukuaji huo.