Uchumi wa Kenya waimarika

Rais Uhuru Kenyatta akiwa na Waziri wa Mambo ya Nje, Amina Mohamed.

Ripoti iliyochapishwa kwenye gazeti la Nation Jumanne inasema kuwa uchumi wa Kenya umekuwa kwa asilimia 5.6 katika mwaka wa 2015 ilkilinganishwa na asilimia 5.3 mwaka uliotangulia. Sekta ya utengenezaji bidhaa imekua kwa asilimia 3.5 kutokana na kushuka kwa bei za mafuta ulimwenguni.

Kwenye mtandao wa Twitter, waziri wa mambo ya nje wa Kenya Balozi Amina Mohamed anasema kuwa uchumi huo utaimarika hata zaidi kwa kiwango cha asilimia 6.6 katika mwaka wa 2016.