Harris amteua Walz kuwa mgombea mwenza

FILE - Gavana wa Minnesota Tim Walz

Makamu wa Rais Kamala Harris amemteua Gavana wa Minnesota Tim Walz kuwa mgombea mwenza katika uchaguzi mkuu wa mwezi Novemba.

Uteuzi wa Walz, mwenye umri wa miaka 60, umefanyika muda mfupi baada ya kamati ya kitaifa ya chama cha Democratic kutangaza Harris kuwa mgombea wa urais wa chama hicho kufuatia upigaji kura uliofanyika kwa njia ya mtandao Jumatatu usiku.

Mgombea wa urais kwa tiketi ya chama cha Republican Donald Trump na mgombea mwenza JD Vance wameimarisha kampeni katika jimbo la Minnesota anakotoka Tim Walz. Hakuna mgombea wa urais wa chama cha Republican ameshinda Minnesota kwa zaidi ya miaka 50.

Walz amekuwa gavana wa Minnesota tangu mwaka 2018 alipogombea nafasi hiyo kwa mara ya kwanza kabla ya kushinda tena mwaka 2022.

Amesifiwa kwa kuanzisha sera za maendeleo kama mpango wa chakula kwa wanafunzi shuleni, kuruhusu matumizi ya bangi, kulinda haki ya utoaji mimba na kuweka mikakati ya kudhibithi matumizi ya bunduki.

Alikuwa mwalimu wa Geografia katika shule ya upili na mwanajeshi kwa muda wa miaka 24.

Kama kiongozi wa muungano wa magavana wa chama cha democratic, amekuwa mtetezi mkubwa wa utawala wa rais Joe Biden na Kahama Harris.

Ana msimamo wa wastan kuhusu ndoa za watu wa jinsia moja, anaunga mkono haki ya mwanamke kutoa mimba, matumizi ya bunduki, upatikanaji wa matibabu kwa bei rahisi, wafanyakazi kujiunga na miungano, wafanyakazi kupata likizo ya kimatibabu au kuhudumia familia. Hizi sifa zinatosha kwa wapiga kura Marekani kumuunga mkono.