Baadhi ya maduka nchini Tunisia yanapunguza mgao wa bidhaa ikiwa ni pamoja na mafuta ya kupikia, sukari na siagi, huku foleni kubwa ikionekana kwenye vituo vya petroli kutokana na uhaba wa mafuta huku serikali ikikabiliana na msukosuko wa fedha za umma.
Baadhi ya maduka ya chakula yameweka ukomo kwa wateja kununua paketi moja tu kwa bidhaa ambazo ni chache, wakati foleni nje ya vituo vya petroli zimezuia usafiri wa magari katika sehemu za mji mkuu.
Rais Kais Saied na serikali yake hawajazungumzia kuhusu uhaba huo isipokuwa kwa kutangaza nia ya kuwalenga walanguzi na wale wanaoficha bidhaa. Hata hivyo, Saied siku ya Ijumaa alimfukuza kazi mkuu wa kampuni ya usambazaji bidhaa za petroli y Tunisia.