Russia inakabiliwa na ongezeko la kulaaniwa kimataifa huku kukiwa na ripoti za uwezekano kuwa majeshi ya Russia yametenda uhalifu wa kivita katika viunga vya Kyiv vya Bucha na sehemu nyingine nchini Ukraine.
Katika ujumbe wa Twitter wa Aprili 3, Rais wa Baraza la Ulaya Charles Michel alisema Moscow itakabiliwa “na vikwazo zaidi vya Umoja wa Ulaya.”
Michael alisema “ameshtushwa na picha za ukatili uliotendwa na majeshi ya Russia huko Kyiv mkoa ambao umekobolewa.
Waziri wa Mambo ya Nje wa Uingereza Liz Truss alisema katika taarifa yake kuwa serikali yake imeona “ongezeko la ushahidi wa vitendo vya kuhuzunisha vilivyofanywa na majeshi ya uvamizi katika miji kama vile Irpin na Bucha.”
Meya wa Bucha Anatoly Fedoruk alisema Aprili 2 kuwa kiasi cha raia 300 katika eneo hilo walipigwa risasi wakati mji huo ulipokuwa unakaliwa kimabavu na majeshi ya Russia. Watu wapatao 280 wanadaiwa kutupwa
Picha za video na zisizo za video za miili ya watu hao zimesambazwa kwenye mitandao ya kijamii.
“Kutakuwa na hatua zitakazo chukuliwa kwa uvamizi wa Russia,’ Fedoruk amekaririwa akisema.
Russia haijajibu ripoti hizo.
Meya wa Kyiv Vitali Klitschko ameliambia gazeti la Ujerumani Bild kuwa “ kile kilichotokea huko Bucha na viunga vya Kyiv kinaweza tu kuelezewa kama ni mauaji ya kimbari.” Amesema Rais wa Russia Vladimir Putin anawajibika.
Waziri wa Mambo ya Nje wa Ukraine Dymtro Kuleba alisema kuwa” mauaji ya Bucha yalifanywa kwa makusudi.”
“Ninataka vikwazo vipya vikali viwekwe hivi na G7,” Kuleba aliandika Aprili 3 katika Twitter, akielezea kundi hilo la nchi saba zenye uchumi unaongoza duniani.