Rais Trump asema UN inakabiliwa na urasimu

Rais Donald Trump akiwa na balozi Nikki Hailey

Rais wa Marekani Donald Trump amefungua duru ya majadiliano  ya pamoja katika Umoja wa Mataifa (UN) Jumatatu, siku ya kwanza ya mkutano wa kidiplomasia wa siku nne huko New York, Marekani.

Hiki ni kikao cha kila mwaka cha Baraza Kuu la UN na mikutano mingine ya pembeni ambayo inaendelea huko New York.

Akionekana kwa mara ya kwanza kwenye mkutano huo siku moja kabla ya kufunguliwa rasmi kwa kikao cha baraza kuu Rais Trump aliongoza kikao kuhusu mageuzi katika taasisi hiyo ya dunia na kutaka hatua za kijasiri zichukuliwe kuifanya taasisi hiyo yenye mataifa wanachama 193 iwe taasisi yenye nguvu na amani.

Rais Trump (C) na wanadiplomasia katika UN

Akizungumza pamoja na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Guterres na balozi wake katika Umoja wa Mataifa, Nikki Haley, Rais Trump aliwaambia wanadiplomasia kwenye mkutano wa mageuzi kwamba taasisi hiyo haifanyi vizuri kama inavyotakiwa na kwamba urasimu ndio wa kulaumiwa. Alisema viongozi wa dunia lazima wasizuiwe katika kutumia njia za zamani.