Theluthi moja ya warundi wanahitaji msaada wa chakula:OCHA

Ripoti ya OCHA inasema warundi wanahitaji msaada wa chakula

Ripoti ya mashirika ya kimataifa ya kutoa misaada nchini Burundi-OCHA iliyotolewa Jumatatu inasema theluthi moja ya warundi wanahitaji misaada ya dharura kwa mwaka huu wa 2018.

Katika mkakati wake wa kusaidia waathirika hao OCHA inasema fedha inayohitajika ni dola milioni 141 za kimarekani ili kukidhi mahitaji yao ambapo mwaka jana walihitaji dola milioni 73 kuwasidia watu milioni tatu waliokuwa katika hali mbaya ya kibinadamu.

Ripoti hiyo inadai kuwa idadi ya waathiriwa inadizi kuongezeka kila mwaka tangu mwaka 2016. Ifuatayo ni taarifa ya mwandishi wetu wa Bujumbura, Haidallah Hakizimana.

Your browser doesn’t support HTML5

Taarifa ya Haidalla Hakizimana wa Bujumbura, Burundi