Texas: Wabunge wa Marekani waeleza nini kifanyike kukabiliana na mauaji nchini

Your browser doesn’t support HTML5

Gavana wa jimbo la Texas Greg Abbot anasema watu 19 waliuawa Jumanne katika shambulio la risasi kwenye shule moja ya msingi.

Abbot anasema mshukiwa wa shambulio hilo, kijana mwenye umri wa miaka 18, amefariki pia na anaaminika kuuawa na maafisa wa usalama.

Anasema watoto wa shule 14 na mwalimu wao waliuawa jana Jumanne kwenye shule ya msingi ya Robb huko Uvalde, umbali wa maili 85 kutoka mji wa San Antonio.

Shambulio hilo la Texas linajiri chini ya wiki mbili baada ya mwanaume mzungu mwenye umri wa miaka 18 kufyatua risasi kwenye duka la chakula mjini Buffalo jimbo la New York na kuua Wamarekani weusi 10, shambulio ambalo lilitajwa na maafisa kuwa la chuki ya ubaguzi.