Sudan yakataa uraia wa nchi mbili na Sudan Kusini

Picha ya mji mkuu Khartoum Sudan

Watu wengi wa Sudan kusini walikimbilia Kaskazini wakati wa vita vya wenyewe kwa wenye vilivyodumu kwa miaka 21

Chama tawala cha Sudan kimethibitisha kuwa serikali haiwezi kutoa uraia wa nchi mbili kwa watu wa Sudan Kusini baada ya nchi hiyo mpya kusema kuwa itaruhusu uraia wa nchi mbili.

Uraia ni suala kuu linalotakiwa kupatiwa ufumbuzi baada ya nchi hizo mbili kujitenga julai tisa.

Msemaji wa chama cha Sudan National Congress , Ibrahim Ghandur amesema serikali haiwezi kuongeza muda wa uraia wa nchi mbili kwa Sudan Kusini kwa sababu raia wa nchi hiyo walipiga kura kwa wingi kujitenga na upande wa kaskazini.

Ghandur pia alisema Ikiwa Sudan kusini itaruhusu uraia wa nchi mbili mamilioni ya watu wa Sudan Kusini watabaki Sudan Kaskazini na kuacha chama tawala cha Sudan kuwa msimamizi wa vyanzo vya asili na kuwa watu wachache. Watu wengi wa Sudan kusini walikimbilia Kaskazini wakati wa vita vya wenyewe kwa wenye vilivyodumu kwa miaka 21 ambavyo viliharibu eneo kubwa la Kusini.